Kamanda wa Kanda Maalum DSM Jumanne Muliro amesema wanawashikilia watu 14 akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman MBOWE, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na Mwenykiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Godbless Lema.
Kamanda Muliro amesema hayo mbele ya waandishi wa habari hii leo Septemba 23 tarehe tajwa ya maandamano hayo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam.