MAANDAMANO CHADEMA: Hali ilivyo Mwenge, Ubungo jijini Dar es Salaam

Dar es Salaam. Leo Jumatatu, Septemba 23, 2024, ikiwa siku ya maandamano ya maombolezo na amani yaliyotangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hali ya eneo la Mwenge, huku askari polisi wakifanya doria kila sehemu na kuegesha magari yao pembeni mwa barabara.

Askari hao baadhi wapo kwenye magari mawili ya polisi na wengine wakiwa kwenye gari la kuwasha. Wapo wenye silaha za moto na virungu wakitembea huku na kule kuhakikisha usalama eneo hilo unaimarika.

Si eneo la Mwenge pekee, kwani hata katika mataa ya daraja la Kijazi, Ubungo hali ni kama hiyo, huku baadhi ya askari wakikataza watu na bodaboda kusimama maeneo hayo, licha ya kuwepo abiria wanaosubiri usafiri na kutakiwa kwenda katika vituo husika.

Hali hiyo ya kuzuia watu wasisimame eneo hilo, limeogopesha watembea kwa miguu, kwani wapo ambao hawajui kama kuna maandamano.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts