Makocha, Waamuzi  judo wanolewa kimataifa

MAKOCHA na Waamuzi30 wa mchezo wa judo wameanza mafunzo ya kimataifa ya mchezo huo ya level one.

Miongoni mwa washiriki ni nyota wa timu ya taifa, Andrew Thomas, Anangisye Pwele, Abou Mteteko na mwanadada, Asiatu Juma.

Mafunzo hayo ya siku 10, yameanza Septemba 22, 2024 kwenye  kituo cha

Olympafrica kilichopo Kibaha Mkuza, mkoani Pwani.

Mwenyekiti wa Chama cha Judo Tanzania (Jata), Zaid Hamis amesema mafunzo hayo ndiyo msingi wa mchezo huo nchini kwani yanakwenda kuwaandaa makocha na marefa kufundisha na kuchezesha katika timu za vijana.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na kudhaminiwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) kupitia kitengo chake cha misaada (Olympic Solidarity) yanatolewa na mkufunzi Erdan Dogan kutoka Uturuki.

Zaidi amesema lengo ni kuhakikisha wanapata marefa na makocha ambao watakwenda kufundisha mchezo huo shuleni.

“Mchezo wetu umeanza kusambaa na kuchezwa na vijana, hivyo ili ufike mbali zaidi, Jata kwa kushirikiana na TOC tumefanya mafunzo kwa makocha na marefarii 30 ambao watakwenda kufundisha timu za vijana,” amesema.

Akifungua mafunzo hayo, rais wa TOC, Gulam Rashid amesema kama yakitumika ipasavyo yanakwenda kujenga msingi imara kwenye timu za vijana.

“Timu za vijana ndiyo msingi wa timu ya wakubwa, mkienda kuwaendeleza vijana baada ya mafunzo haya mtatengeneza wigo mpana wa kupata timu ya taifa baadae.

Related Posts