Mpango shirikishi kwenye kilimo nchini wazinduliwa

Taasisi ya kilimo Tanzania, Africa Food hivi karibuni ilizindua mpango kabambe na wa kimkakati wa kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo kwa mtindo wa ushirikishwaji kwa wadau wote wa kilimo nchini ili kuleta tija kwenye sekta hiyo.

Akizungumza na kwenye uzinduzi rasmi wa mpango huo, Mbunge wa Jimbo la Mahonda , Mkoani Kaskazini B, Mheshimiwa Abdullah Mwinyi alisema kwamba mpango huo utaleta tija kwa kufungua fursa kwa wakulima kuanza kushirikiana na wadau wengine kwenye kilimo hapa nchini.

“Mpango huu ni shirikishi kwa kufungua milango kwa wakulima wadogo kushirikiana wadau wengine kwenye sekta ili kuchochea mnyororo wa thamani na kufungua fursa ya kuongeza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na kupata ziada kwenye chakula,” alisema

Aliongeza kwamba madhumuni ya mpango huu ni kuiwezesha jamii, kuhimiza ubunifu, na kukuza mbinu endelevu katika kuleta mapinduzi kwenye sekta za kilimo, uvuvi na mifugo barani Afrika.

“ Idadi ya watu hapa nchini inazidi kuongezeka na ni fursa adhimu kwa wakulima na wadau wengine kuweka nguvu kwenye kilimo maana ndio mkombozi wa kweli wa kiuchumi na fursa zingine zipo ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na idadi ya watu wasiopungua 250 Millioni ndani ya Afrika ni fursa adhimu kwa wakulima na wadau wengine kwenye sekta ya kilimo,”

“Cha muhimu ni kutoa elimu ya kutosha kwa watanzania kuhusu mpango huu na kuhakikisha tunakuza mnyororo wa thamani na lazima tuanze kutizama fursa ya kuuza nje ya hapa nyumbani na kwenye soko la Afrika Mashariki,” aliongeza

Kwa Upande Mkurugenzi wa Africa Food , Bw Herment Mrema alisema kwamba mpagngo huu ni mpya hapa nchini na lengo kuu ni kumshirikisha mkulima ili aweze kuongeza kipato na awe mwekezaji kupitia shamba lake mwenyewe.

“Mpango unafungua fursa kwa mkulima kuwa mwekezaji kwa kuamua kukodisha shamba lake ambapo wadau wengine wataleta watalaamu wa kupima udongo , kuleta mbolea , mbegu na vitendea kazi na kutafuta masoko na kuchochea mnyororo wa thamani mpaka kiwandani ,” alisema Bw Mrema

Alisema kwamba mpango huu utaleta mapinduzi makubwa pamoja na mambo mengine utawavutia vijana kwenye kilimo na kupunguza tatizo la ajira hapa nchini na kuongeza kipato wa wadau wote watakaoingia kwenye mpango shirikishi.

Alifafanua kwamba kwenye mpango huo utafungua milango kwa Taasisi za kifedha kuja kushirikiana na wadau wote pamoja wakulima wadogo wadogo kwa kuleta mitaji na bima ili kuwa na uhakika wa kilimo endelevu.

Kwa upande wake , Mkurugenzi Mtendaji AfricaFood, Bw Godwin Nyelo alisema kwamba siyo tu ni mradi—ni harakati zinazolenga kuonyesha uwezo mkubwa wa sekta ya kilimo kujitosheleza katika uwepo na usalama wa chakula katika bara la Afrika.

Aliongeza kwamba mpango huo unaandaa mazingira wezeshi ambapo kila mkulima, mjasiriamali, na jamii, wanapata nguvu ya kuchangia uchumi wa kilimo unaojitegemea na kustawi kwa maslahi ya wote.

Bw Nyelo alisema pamoja na mambo mengine lengo la mpango huo ni kupunguza kwa na hatimaye kumaliza kabisa uagizaji wa chakula na upotevu, na kuifanya Tanzania na Afrika kuwa na kilimo endelevu, huku ukihakikisha usalama wa chakula na kuhifadhi urithi wa kitamaduni na mazingira.

“dhamira kuu ya Mpango wa AfricaFood ni kuwawezesha bodi za ushauri za kijamii na wataalam wa ndani kote barani Afrika. Bodi na wataalam hawa watawezeshwa kwa kutumia zana muhimu, maarifa, na msaada ili kuleta mabadiliko. Kupitia mafunzo ya uongozi, ugawaji wa rasilimali, na ushirikishwaji wa jamii, Mpango huu unapanda mbegu za uvumbuzi na uongozi zitakazochochea maendeleo barani Afrika,” alisema .

Mpango wa AfricaFood unajenga mtandao wenye nguvu wa ushirikiano wa nchi na nchi. Mtandao huu utashirikisha maarifa, kugawana rasilimali, na kushirikishana mbinu bora kote Afrika, kuhakikisha kuwa mafanikio yanasambazwa kwa maendeleo endelevu na changamoto zinashughulikiwa kwa pamoja. Mikutano ya kanda, warsha, na jukwaa la kidijitali

Taasisi imejipanga kutoa elimu kwa wakulima na wadau wengine kuhusu mpango huo shirikishi kwa watanzania ili kujenga uelewa wa pamoja ili kuweza kukuza maendeleo ya kilimo hapa nchini.

Related Posts