Dar es Salaam. Mtoto wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Nicole Mbowe amekamatwa na Polisi leo Jumatatu Septemba 23, 2024 eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam akifanya mahojiano na waandishi wa habari.
Nicole amekamatwa na polisi, ikiwa muda mfupi baada ya baba yake, Freeman Mbowe kukamatwa eneo hilo hilo la Magomeni.
Septemba 11, 2024 Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na kuuawa, akiwemo aliyekuwa kada wake, Ali Kibao. Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.
Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo wa suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi