Polisi wasema wamekamata 14, akiwamo Lema maandamano ya Chadema

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wanawashikilia watu 14, wakiwemo mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti-Bara, Tundu Lissu na mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini, Godbless Lema.

Muliro amesema watu hao wamekaidi amri halali ya Polisi ya kuacha kushiriki maandamano, jijini Dar es Salaam na mahojiano dhidi yao yanaendelea.

Kamanda Muliro amesema hayo leo Jumatatu, Septemba 23, 2024 alipozungumza na waandishi wa habari alipotoa taarifa ya kinachoendelea juu ya maandamano ya maombolezo na amani yaliyoitishwa na Chadema.

“Polisi linauhabarisha umma kuwa watu hawa wamekamatwa na wanahojiwa,” amesema Kamanda Muliro.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts