Rais Samia akagua ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Songea

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua na kupokea taarifa ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Songea ambao umekamilika kwa asilimia 100% Mkoani Ruvuma.

Rais Dkt. Samia amekagua kiwanja hicho, leo September 23, 2024 mara baada ya kuwasili Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi ya miradi na kuongea na Wananchi.

Rais Dkt. Samia amepokea taarifa ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Songea uliohusisha upanuzi na kuongeza urefu wa barabara ya kuruka na kutua Ndege, ujenzi maegesho mapya ya Ndege (Apron), ujenzi wa barabara moja ya kiungio, ujenzi wa mnara wa Waongoza ndege (Control Tower), kuimarisha maeneo ya usalama kiwanjani pamoja na ununuzi, usimikaji wa taa za kuongozea ndege na gari la zimamoto.

Akitoa taarifa mbele ya Rais, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali ilitoa kiasi cha Tsh. bilioni 40.87

Related Posts