Rais Samia ziarani mkoani Ruvuma

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan ametembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji iliyopo Mjini Songea mkoani Ruvuma kwa lengo la kutoa heshima ya kumbukizi ya mashujaa wa vita ya Majimaji vilivyoanza mwaka 1905-1907, huku akiweka shada la maua katika kaburi la Chifu Msaidizi wa Wangoni Nduna Songea Mbano.

Rais Samia ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambapo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi

Pia Rais Samia ametembelea ukumbi wa historia ya vita ya Maji Maji, onesho la nyumba ya Inkosi ( Chifu) wa Kabila la Wangoni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa na watoto wawili juu ya gari wakiwapungia mkono Wananchi wa Songea mara baada ya kufunga Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa lililofanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Songea Septemba 23, 2024.
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akicheza mchezo wa bao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho katika uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma Septemba 23, 2024.

Related Posts