Wakili Mwasipu: Lissu anatuhumiwa kuhamasisha vurugu maandamano ya Chadema

Dar es Salaam. Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu amesema Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu anashikiliwa kituo cha Polisi Mbweni, Dar es Salaam akituhumiwa kuhamasisha watu kufanya vurugu kupitia maandamano yaliyoitishwa na chama hicho.

Lissu ni miongoni mwa viongozi na wanachama zaidi ya 40 wa chama hicho, akiwamo mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, waliokamatwa kwa nyakati tofauti leo Jumatatu, Septemba 23, 2024.

Lissu alikamatwa leo saa 4 asubuhi, baada ya maofisa wa Polisi waliozingira nyumba yake maeneo ya Tegeta na kisha kumpeleka kituo cha polisi Mbweni.

Akizungumza na Mwananchi nje ya kituo hicho cha polisi, Wakili Mwasipu amedai wamemtajia (Lissu) kosa la kuhamasisha watu kufanya maandamano haramu.

“Ametajiwa kosa la kuhamasisha watu kufanya vurugu kupitia maandamano haramu,” amedai Wakili Mwasipu.

Amesema baada ya kuandika maelezo amerudishwa mahabusu. “Tunasubiri dhamana, maana askari aliyeandika maelezo amesema anasubiri maelekezo kutoka juu,” amesema

Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi

Related Posts