Dar es Salaam. Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu amesema Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu amekamatwa na polisi asubuhi ya leo Jumatatu, Septemba 23, 2024.
“Lissu amekamatwa nyumbani kwake Tegeta na amepelekwa Kituo cha Polisi Mbweni na mimi kama wakili niko njiani nakwenda huko kujua sababu za kukamatwa kwake,” amesema Hekima alipozungumza na Mwananchi.
Jitihada za kulipata Jeshi la Polisi zinaendelea.
Lissu amekamatwa saa chache kabla ya kuanza kwa mandamano waliyoyaitisha ya maombolezo na amani, jijini Dar es Salaam.
Endelea kufuatilia Mwananchi