Bodaboda 600 washiriki maandamano ya amani wilaya Mlele mkoani Katavi

Zaidi ya maafisa wasafirishaji kwa kutumia pikipiki maarufu kama bodaboda mia sita (600) wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamefanya paredi maalum iliyotambulika Samia Bodaboda Day Kwa kupita kwenye mitaa mbalimbali kuanzia ofisi ya mkuu wa Wilaya hadi uwanja wa shule ya Iyonga.

Paredi hiyo ambayo imeongonzwa na Mkuu wa Wilaya ya Melele Alhaj Majid Mwanga na mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Mlele Bi. Sigilinda Mdemu huku lengo kuhamasisha vijana kushiriki kujiandikisha kwenye orodha ya daftari la mpiga kura zoezi litakalo anza actoba 11 hadi 20 mwaka ikiwa maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa,viongoji na vijiji novemba 27 mwaka huu

Maadhimisho hayo yalifanyika kwa kufanyika ikiwa na lengo la Serikali kutambua na kuthamini shughuli za vijana wa Bodaboda ndani ya wilaya hiyo kwenye shughuli za uchumi na ulinzi na amani.

Akizungumza na vijana hao wa bodaboda mkuu wa Wilaya hiyo Majid Mwanga amewataka vijana kuacha kubaki nyuma katika masuala ya mbalimbali ya kiserikali kwani wao ndio tegemeo kubwa kwa taifa.

Amesema ili Taifa liendelee linahitaji vijana wenye afya njema na kujitoa hivyo uchaguzi wa serikali za mitaa ni moja ya suala muhimu hivyo kundi hilo linatakiwa kuwa mstari mbele kuhamasisha vijana wengine na Watu wote kwa ujumla katika.kushiriki.

“tumewashirikisha bodaboda Kwa sababu wanawafikia Watu wengi zaidi mfano kwa siku akibeba abiria 7 Kwa mwezi anabeba abiria 210 hapa tuna bodaboda 600 hivyo watawafikia Watu zaidi ya 120,000 kwa mwezi mmoja”

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji halmashauri Bi Sigilinda Mdemu amesema wamejipanga kutoa elimu kw mpiga kura kwenye maeneo yote ya mikusanyiko Kwa kuanzia na vijana ,wanawake na walemavu ili makundi yote wapate fursa ya kushiriki bila changamoto yoyote.

Akizungumza Kwa niaba ya bodaboda zaidi ya mia sita mwenyekiti wa bodaboda Ignasi Kilanga
amesema wamefurishwa na kitendo cha Serikali kutambua umuhimu wao na kuwashirikisha katika masuala muhimu ya uchaguzi na wapo tayar kuwa mabalozi Kwa wengine.

Amesema hawapo tayari kutumika Kwa baadhi ya Watu wenye Nia ovu Kwa kufanya jambo lolote la kuhatarisha amani katika jamiii hasa wakati wa mchakato mzima wa kupiga kura uchaguzi w. Serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu mwakani
.
Viajana wa Bodaboda katika kushereheke siku yao hii muhimu waliweza kugawa kwa wagonjwa vitu mambali mbali kama sabuni kituo cha Afya Inyonga ikiwa ni zawadi kwa wakazi wa Inyonga
Pia walitoa damu kwaajili ya wahonjwa wanohitaji damu hospital ikiwa ni wamama wajawazito na wanaopata ajali.

Related Posts