KOKA ACHAGIZA ML.5 KUSAIDIA MATUNDU YA VYOO SHULE YA SAINI VISIGA

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu ametumia fedha za mfuko wa Jimbo kiasi cha shilingi milioni tano katika mradi wa ujenzi wa shule ya msingi shikizi ya Saini iliyopo kata ya Visiga ili kuondokana na changamoto ya wanafunzi wadogo kutembea umbari mrefu wa zaidi ya kilometa 12.

Hayo yamebainishwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mathias Alexanda wakati akitoa taarifa kwenye ziara ya kikazi ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini ambaye alifika kwa ajili ya kuweza kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu pamoja na miundombinu ya barabara.

Mkuu huyo amebainisha kwamba shule hiyo ambayo imeanzishwa mwaka huu imeweza kuwa ni msaada mkubwa kwa watoto wadogo wenye umri wa kuanzia miaka mitano na kuendelea kwani hapo awali wanafunzi hao walikuwa na adha kubwa ya kutembea umbari mrefu kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo wa shule mwaka huu.

Mkuu huyo amempongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano ambayo imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha miundombinu ya matundu ya vyoo pamoja na miundombinu mingine ya madarasa katika shule hiyo.

Mkuu huyo hakusita kuishukuru Halmashauri ya mji Kibaha kwa kuweza kuwa bega kwa bega katika kuchochea maendeleo ya elimu pamoja na Diwani wa Kata ya Visiga kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa shule.

Aliongoze kuwa katika mradi huo serikali imeweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 62 ambazo zimeweza kusaidia kwa kiwango kikubwa katika ujenzi wa kuanzishwa kwa shule hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amebainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuweka mikakati madhubuti ambayo itaweza kusaidia katika kuboresha sekta ya elimu hivyo ameamua kuchangia fedha hizo ili kuwaondolea wanafunzi hao kutembea umbari mrefu.

“Kikubwa nimefarijika kufanya ziaara ya kikazi katika kata ya Visiga na nimetembelea katika shule hii ya awali na darasa la kwanza na la pili la Saini na nimeweza kujionea mradi huu umeanza utekelezaji wake na ujenzi wa baahi ya madarasa na mimi nimeweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu ikiwemo madarasa pamojana matundu ya vyoo.

Aidha Mbunge Koka amebainisha kwamba kipaumbele chake kikubwa katika mfuko wa Jimbo ni kuhakikisha kwamba anaboresha zaidi shule ambazo zipo pembezoni ikiwemo kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuweza kuboresha zaidi miundombinu ya madarasa pamoja na maboma ambayo miundombinu yake imechakaa.

Naye Afisa mtendaji wa Kata ya Visiga Aloise Nyello amesema kwamba serikali katika kutekeleza elimu bure malipo imetoa kiasi cha shilingi milioni 292 kwa ajili ya shule za msingi na sekondari.

Mbunge Koka yupo katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi.


 

Related Posts