JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetoa wito kwa vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani kuomba nafasi za kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kujitolea katika mwaka wa fedha 2024 huku ikisisitizwa kuwa nafasi hizo utolewa bure kabisa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, iliyosomwa leo tarehe 25 Septemba 2024 na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Juma Mrai mbele ya vyombo vya habari amesema kuwa JKT inawataarifu Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na Jeshi hilo kwa mwaka 2024 ambazo utolewa bure.
Amesema kuwa utaratibu wa vijana hao kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo,unaratibiwa na ofisi za Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ambako mwombaji anaishi.
“Usahili wa vijana hao kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe Mosi Oktoba 2024 kwa Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani.
“Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia Mosi Novemba 2024 hadi tarehe 3 Novemba 2024.
“Aidha Jeshi la Kujenga Taifa linapenda kuwataarifu vijana watakaopata fursa hiyo kuwa Jeshi la Kujenga Taifa kuwa halitoi ajira,wala halihusiki kuwatafutia ajira katika asasi,vyombo vya ulinzi na usalama na Maahirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo kuwa kiserikali.
“Bali utoa mafunzo ambayo yatasaidia vijana kukiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na Jeshi la kujenga taifa,” ameeleza Kanali Mrai.
Akiendelea kufafanua Kanali Mrai amesema kuwa sifa za mwombaji na maelekezo ya vifaa vinavyotakiwa kwenda navyo yanapatikana katika Tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz.
“Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduki Mabele,anawakaribisha vijana wote watakao pata fursa hiyo,kuja kujiunga kujiunga na vijana wenzao ili kujenhewa Uzalendo,Umoja wa Kitaifa, Ukakamavu, kufundishwa Stadi za kazi, Stadi za Maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao,” ameeleza Kanali Mrai.