Ameyasema hayo leo Septemba 25,2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafamasia Duniani ambayo ni maalumu kwa wafamasia ulimwenguni kote na inalenga kuongeza uelewa wa umma kuhusu jukumu muhimu la wafamasia katika huduma za afya.
Amesema Wafamasia wanatumika kukuza uzuiaji wa magonjwa, kama vile kutoa chanjo, kufanya uchunguzi wa afya, kuelimisha wagonjwa, na kusaidia kuboresha elimu ya afya katika sehemu husika.
Aidha amewakumbusha wafamasia wote kwenye siku yao hii muhimu kuwa wafamasia wanatakiwa kuongoza katika uangalizi wa dawa, kwa mfano, kuhakikisha usalama na ufanisi wa antibiotics na madawa mengine na namna ya kutoa miongozo ya matumizi ya dawa sahihi kuepuka usugu wa magonjwa kutokana na matumizi matumizi mabaya ya dawa.
Naye Msajili wa baraza la Famasi Tanzania Boniface Magige katika siku hii ya wafamasia duniani ametoa rai kwa wafamasia na wamiliki wa maduka ya dawa waotoa dawa kwa mgonjwa asiyekuwa na cheti cha daktari,kwani kufanya hivyo ni kuendeleza tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa na kuhatarisha afya za watu.
Pia amewataka Watanzania kuacha matumizi holela ya dawa bila kufuata ushauri wa Madaktari ili kuepuka usugu wa dawa dhidi ya vimelea ambapo husababisha dawa hizo kushindwa kufanya kazi yake.
“Watu wanao fungua maduka ya dawa za binadamu bila kufuata sheria Serikali itawachukulia hatua kali dhidi yao”
“Mtindo uliozoeleka, ni kwenda kwenye duka la dawa, kununua au kueleza shida yako. Na bila kujali, mwingine humeza vidonge vichache na baadhi hutumia nusu dozi na kuachana na dawa baada ya kupona,tuache tabia hii na tupime kwa usahihi na kupewa dawa sahihi”
Baraza la Famasi linatahadharisha watu kuepuka kununua dawa kwenye maduka yasiyosajiliwa sajiliwa kisheria, kwa kuwa ubora wake si uliokubalika ,pia maelezo ya matumizi yanaweza kutolewa bila usahihi au na mtu asiye sahihi, kitendo kinachoweza kusababisha madhara kwa mtumiaji.
Amemaliza kwa kusema baraza la Famasi lililopo chini ya Wizara ya Afya, linaelimisha matumizi sahihi ya dawa na hugeuka kuwa sumu na huleta madhara iwapo hazitatumiwa ipasavyo hivyo ni muhimu mgonjwa kufanyiwa uchunguzi na kupata ushauri wa mtaalam wa afya kabla ya kutumia dawa.
Naye Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Mashariki Adonis Bitegeko amesema kuwa mamlaka itaendelea kupambana na usugu wa vimelea vya Dawa na kuelimisha jamii katika kuhakikisha Dawa zinatumika kwa ufasaha na usahihi kwakufuata maelekezo sahihi ya Kitaalam.
“Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ina wajibu wa kulinda afya ya jamii kwa kuhakikisha ubora na usalama wa dawa na vifaa tiba”
“TMDA pia inasimamia Usajili wa majengo na ukaguzi,udhibiti wa uingizaji na usafirishaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi,kuteketeza bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora na usalama,uchunguzi wa sampuli katika Maabara ya TMDA pamoja na ufuatiliaji wa ubora wa dawa na vifaa tiba na udhibiti wa majaribio ya dawa alisema
Wakati dunia ikiaazimisha siku ya wafamasia mwaka huu wa 2024 bado Dunia inashudia ongezeko kubwa la usugu wa Dawa,Ongezeko la matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari,ongezeka la watu kutumia Dawa bila kupima , huku Watanzania wakitakiwa kubalisha mifumo hiyo ya maisha kuacha kutumia dawa bila kufuata ushauri wa Daktari.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mfamasia Kukidhi Mahitaji ya Kiafya Duniani,” ikisisitiza umuhimu wa wafamasia katika kuboresha afya za watu na jamii kwa ujumla. Siku hii inatoa fursa ya kutafakari kuhusu mchango wa wafamasia na umuhimu wa matumizi sahihi ya dawa.