Kocha Mchenga ataja kilichowatibulia | Mwanaspoti

KOCHA mkuu wa Mchenga Star, Mohamed Yusuph pointi walizofungwa robo ya tatu na JKT ndizo zilizochangia kupoteza mchezo huo kwa vikapu 70-65 licha ya vijana wake kucheza vizuri kwenye Uwanja wa Donbosco Oysterbay.

Katika mchezo huo, timu zote zilianza taratibu huku zikisomana na robo ya kwanza kufungana pointi  21-21.

Hata hivyo, robo ya pili, JKT ikimtumia mchezaji wao, Jonas Mushi iliongoza kwa pointi 15-11, 17-13 na robo ya nne Mchenga Star ikaongoza kwa pointi 21-17.

“Kwa kweli timu yangu ilicheza vizuri hata mashabiki waliokuwepo uwanjani ni mashahidi, ni makosa madogo tu ndiyo yaliyofanya tupoteze mchezo,” alisema Yusuph.

Katika mchezo huo, Baraka Mopere wa JKT alifunga pointi 18, tisa kati ya hizo ikiwa ni mitupo mitatu ‘Three points’, akifuatiwa na Jonas Mushi aliyefunga 15.

Kwa upande wa Mchenga Star, Jordan Jordan alifunga pointi 16, akifuatiwa na Meshack Itenda aliyefunga 15.

Related Posts