KATIKA toleo la 26 Septemba mwaka huu, gazeti la MwanaHALISI liliripoti katika ukurasa wa mbele, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi, anataka Rais Samia abakie madarakani hadi mwaka 2035, lakini mwenyewe amekana kutamka maneno hayo.
Msingi wa habari hiyo ni kipande cha video iliyokuwa ikizunguka mitandaoni ikimuonyesha kiongozi huyo akiwa kwenye mkutano.
MwanaHALISI Online, imeona video inayomuonyesha Waziri Lukuvi akizungumzia jambo hilo, lakini baada ya uchunguzi wake imebaini kutokana na ukuaji wa teknolojia ya kisasa, kuna kila dalili kuwa imehaririwa kwa nia mbaya.
Baada ya majadiliano ya kina na Waziri Lukuvi, tumekubaliana kwa kuchapisha maudhui hayo, tumemkosea na kwa sababu hiyo tunamuomba radhi yeye na wote walioguswa na habari tuliyoandika.
Tunaamini kila mmoja wetu ana wajibu wa kuhakikisha Katiba na sheria zilindwa kwa nguvu na thamani kubwa.
Mhariri.