Dar es Salaam. Serikali imetangaza nafasi zaidi ya 800 za ajira katika kada mbalimbali ikiwemo ualimu, udereva, utaalamu misitu pamoja na watendaji wa vijiji.
Nafasi hizo ni kutoka halmashauri tatu za wilaya za Kakonko, Mbulu, Iringa, mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nafasi (600) pamoja na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wanaohitaji watu 252.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Serikali imetangaza nafasi (5) za Mtendaji wa Kijiji, dereva daraja la II (2), msaidizi wa kumbukumbu daraja II nafasi (5), mwandishi mwendesha ofisi daraja la II nafasi (2). Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 30, 2024.
Kwa Halmashauri ya Mbulu, nafasi ya Mtendaji wa Kijiji daraja III nafasi (20), dereva daraja II nafasi (1), Msaidizi mwendesha ofisi daraja II (3). Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 30, 2024.
Pia, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa nafasi zilizotangazwa ni Mwandishi mwendesha ofisi daraja III nafasi (2), Mtendaji wa Kijiji daraja la III nafasi (15), dereva daraja II nafasi (2), dereva wa mitambo daraja II nafasi (1).
Baadhi ya masharti ya waombaji ni kuwa raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
Vilevile waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao, kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
“Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria/ wakili sifa za jumla za waombaji ambao tayari ni watumishi wa umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
“Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika,” imeandikwa. Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 28, 2024.
Eneo Mamlaka za Serikali za Mitaa nafasi zilizotangazwa 600 ambazo nafasi (17) ni mwalimu daraja III somo la ushonaji, mwalimu daraja la III somo la uashi nafasi (26), ufundi bomba 18, useremala nafasi (18).
Pia eneo lingine ambalo walimu huitajika ni somo la upakaji rangi na uandikaji maandishi nafasi (3), upoaji na video vya hewa (9), michezo (2), somo la usindikaji wa mbao (5), uzalishaji wa chakula (8) na umeme wa magari nafasi (85).
Ulehemu na utengenezaji wa vyuma nafasi 20, ufundi magari nafasi (20), chakula na vinywaji, mauzo na huduma (5), ufundi umeme (20), michezo (8), somo la utengenezaji wa Programu za Tehama (16), somo la sanaa ya uagizaji na utumbuizaji wa muziki (8).
Nafasi nyingine ni ufungaji nishati ya jua (15), afya ya wanyama na uhaulishaji (10), uzalishaji wa kilimo cha bustani (7), uzalishaji wa mazao nafasi (20), uvuvi na usindikaji wa mazao nafasi (10) walimu somo la biashara nafasi( 125).
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hizo 600 ni Septemba 30, 2024.
Kwa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), nafasi zilizotangazwa ni 252 ambazo ni ofisa misitu nafasi (17), mtaalamu wa sheria (1), mtaalamu wa ufugaji nyuki (6) na mtaalamu wa usafirishaji nafasi (2).
Vilevile nafasi za wahasibu nafasi (4), ofisa kilimo (1), mhandisi ujenzi (1), mtaalamu wa ICT (1), mtaalamu wa utalii (3), manunuzi (2) na mkaguzi wa ndani (3).
Katibu muhtasi nafasi (3), ofisa misitu msaidizi (40), ‘Clinic’ ofisa (2), mtaalamu wa tiba (2), mtaalamu msaidizi wa ufugaji nyuki (11), mtaalamu wa ICT( 1), mtaalamu wa maabara (1), mekanika (2), msaidizi wa manunuzi (2), mtunza kumbukumbu nafasi (3) mhasibu msaidizi (3), mtaalamu wa misitu msaidizi (9), dereva (12) na mtaalamu msaidizi wa ufugaji nyuki (10).
“Mlinzi wa misitu (105), msaidizi wa afya (2), mwendesha mitambo (2), wachoraji ramani (1), mtaalamu wa majengo (1). Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 30, 2024,” imeandikwa kwenye tangazo hilo.