Picha: CRDB Benki yafanya Mkutano huu unaolenga kuimarisha Ushirikiano

Ni Benki ya CRDB ambapo Septemba 25, 2024 wakiwa chini ya uongozi wa Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Neema Mori, na Mkurugenzi Mtendaji wetu, Abdulmajid Nsekela, walikutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Citibank kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa 79.

Mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Benki yetu na Citibank. Kati ya mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni kukuza ushirikiano utakaowezesha upanuzi wa Benki ya CRDB katika masoko ya kimataifa, ikijumuisha Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Tukiwa Benki pekee ya Tanzania iliyovuka mipaka na kutoa huduma katika nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mkakati huu wa upanuzi katika masoko mapya unalenga kuimarisha jitihada za Benki yetu katika kukuza biashara za kimataifa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, ili kuleta thamani kubwa zaidi kwa wateja na wadau wetu.

Related Posts