Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa taasisi zinazosimamia maswala ya usafiri majini

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa umoja wa kimataifa wa taasisi zinazosimamia masuala ya usafiri majini pamoja na makubaliano ya Djibouti wa ngazi ya juu utakaoshirikisha mawaziri wa nchi wanachama 21 za Ghuba ya Aden pamoja na magharibi mwa bahari ya hindi.

Hayo yamesemwa manispaa ya Musoma mkoani Mara na kaimu katibu mkuu wizara ya uchukuzi ambaye pia ni mkurugenzi wa usalama na mazingira bi stella kotondo wakati wa utoaji wa elimu ya usalama wa vyombo vya majini kwa taasisi ambazo zinashiriki Maadhimisho ya Siku ya Usafiri kwa Njia ya Maji Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mkendo vilivyopo katika Manispaa ya Musoma.

‘ hivi sasa Tanzania iko kwenye harakati za kuelimisha wananchi wake kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ili waweze kukaa pamoja na kujadiliana namna ya kukabiliana nayo huku wakiendelea na kazi zao za kiuchumi Hivyo Changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya usafiri kwa njia ya maji barani Afrika zinatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo ambao utaanza mwezi Novemba 27 hadi 29 2024,”

TASAC imejidhatiti kuhakikisha huduma za usafirishaji kwa njia ya maji zinatolewa kwa ubora, ufanisi na kwa wakati licha ya huduma za udhibiti kugawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni udhibiti huduma za bandari na udhibiti huduma za usafirishaji kwa njia ya meli.

’Mkutano huu utatoa mwanga na kuimarisha sekta ya Usafiri Majini ikiwemo utatuzi wa matatizo ya mbalimbali kenye bahari ili  kuongeza maendeleo endelevu katika njia ya usafiri majini licha ya changamoto mbalimbali hasa kwa vita zinazoendelea kwenye nchi mbalimbali ambazo ni wageni wa mkutano huu haziwezi kuzuilika’

Akizungumza na waandishi wa habari Bw Timotheo Gambales

Kaimu katibu tawala Mara amewashukuru wana Mara na kuwaasa kuwa limu walioipata iwe chachu yakuleta mabadiliko na kutambua vihatarishi vilivyopo, namna ya kuvidhibiti pamoja na kukabiliana navyo pale inapotokea tatizo bila kuathiri utendaji kazi wa kila siku.

Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TASAC  Bi Judithi Kagongwe pamoja na Bw Hussein ali makame Mkuu wa mafunzo KMKM wasisitiza mipango na hatua za udhibiti wa ajali katika vyombo vya majini kutasaidia kuokoa maisha ya wengi kwa watumiaji wa usafiri majini.

‘Tuhakikishe tunavaa jaketi za uokozi popote tunapofanya shughuli zetu ‘

Jumla ya Taasisi 25 za Serikali na binafsi kutoka Tanzania Bara na Visiwani zinashiriki Maadhimisho ya Siku ya Usafiri kwa Njia ya Maji Duniani sambamba na Miaka 50 ya Tanzania kuwa mwanachama wa Shirika la Bahari Duniani.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa tarehe 26 Septemba, 2024 na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (Mb).23 hSee Translation

 

Related Posts