TBT Queens ilifanya kweli ni baada ya kuifunga timu ya Spides Sisters kwa pointi 54-44, katika ligi ya kikapu ya Mkoa wa kigoma iliyofanyika katika Uwanja Lake Side.
Katibu mkuu wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Kigoma Aq Qassim Anasi, alisema ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo kati Lake Side na Wavuja Jasho.
Alisema timu nane zinashiriki katika mashindano hayo, kati ya hizo tatu zikiwa za wanawake.
Alitaja timu hizo kwa upande wa wanaume ni Kibondo, Kasulu Heat, TBT, Lake Side Spide na Wavuja Jasho.
Kwa upande wanawake ni Lake Side Queens, TBT Queens, na Spider Sister.