Tshisekedi ataka Rwanda iwekewe vikwazo

 

RAIS Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, ametoa wito Jumuiya kwa Kimataifa kuiwekea Rwanda, vikwazo kutokana na kuwaunga mkono waasi wa M-23, wanaoendesha vita mashariki mwa nchi hiyo. NEW YORK, Marekani

Tshisekedi ameitoa kauli hiyo wakati wa mkutano Mkuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York jana.
Tshisekedi ambaye ametaka kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Kongo, amesema uchokozi wa jirani yake unakiuka uhuru wa taifa hilo huku akisisitiza kuwa kuibuka tena kwa kundi la M-23, kumesababisha mgogoro wa kibinadamu ambao haujawahi kushuhudiwa.

Amesema Rwanda ndiyo inayohusika katika kuvuruga utulivu wa nchi hiyo.

Kwa miongo kadhaa sasa, eneo la Mashariki mwa Kongo lenye utajiri mkubwa wa madini, limekuwa kwenye ghasia za makundi yenye silaha ambazo zimesababisha maafa makubwa.

Mbali ya Tshisekedi, viongozi wengine wa Afrika waliyohutubia jana Jumatano ni wa Ghana, Namibia, visiwa vya Ushelisheli, Libya na Madagascar.

Leo viongozi wa wengine wa mataifa ya Afrika watakaopanda jukwaani ni marais wa Malawi, Cameroon, Kenya, Burundi, Gabon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gambia, Lesotho, visiwa vya Comoros, Sudan na Sudan Kusini.

About The Author

Related Posts