Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imefanya kikao cha Baraza la wafanyakazi leo ili kujadili mafanikio, mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa bajeti mwaka uliopita ya 2023/2024.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu Ununuzi na Ugavi Godfred Mbanyi amesema baraza ni chombo kinachoundwa na sheria ya Mahusiano kazini kwa ajili na kuweka mazingira mazuri mahali pakazi ambapo chombo hiki kinawiwa kwa mkataba baina na Menejimenti pamoja na chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi.
Pia amasema baraza la leo limefanyika ili kutathmini utendaji kazi wa bajeti ya mwaka uliopita ya 2023/2024, kisheria na kiutaratibu bajeti yoyote kabla haijahidhinishwa lazima ipitishwe na Balaza la Wafanyakazi sehemu ya kazi.
Mbanyi amesema Bajeti ya mwaka 2023/2024 ilikamilika toka Juni 30 hivyo ni wajibu wa menejimenti kuja kueleza balaza nini mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa bajeti iliyokamilika muda wake.
“Umuhimu wa Mabaraza ya kazi kwanza yanaleta ushirikishwaji wa wafanyakazi sehemu ya kazi hivyo wafanyakazi wanakuwa ni sehemu ya maamuzi katika taasisi, kwaiyo taasisi sio kwamba inakuwa inaongozwa na Menejimenti lakini inakuwa na chombo ambacho kinawakilisha wafanyakazi wote katika taasisi mbalimbali.” Alisema Mbanyi
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo lililofanyika mkoani Morogoro.