VIONGOZI WA DINI WAKEMEA VURUGU KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA

Na Linda Akyoo-Siha

Viongozi wa Madhehemu mbalimbali ya Dini  katika Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro wamesema hawategemei kuona Vurugu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika November 27,2024 bali wanataka kuona Amani ikitawala  na kuvitaka  vyama vyote vyama vya Siasa vitakavyo shiriki  katika chaguzi hizo kuchukuliana kama ndugu.

wametoa kauli hiyo September 26,2024 katika kikao cha Maekelezo kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Mwaka huu hapo November 27.

Wamesema wapiganao wawili lazima ashinde mmoja wapo ashinde hivyo wakamtaka Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Siha kutenda haki kama alivyo aminiwa na Serikali.

Baadhi ya Viongozi  wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki katika Kikao hicho kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ACT Wazalendo na Chama cha Mapinduzi CCM wamesema hawataki kuona yale yote yaliyojitokeza katika Chaguzi wa Mwaka 2019 na kikubwa ni kuheshimiana , busara hekima na kila chama kitasimanisha mgombea ambaye anakubalika katika jami pamoja na kutoa ushirikiano kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi huo.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha Dkt Haji Mnasi amesema kwa mujibu wa kanuni ya 13 Namba 571 wakazi wote wenye umri wa miaka 18 au zaidi na waliokidhi masharti ya kisheria wanahimizwa kushiriki katika uchaguzi huo.

Aidha Mnasi akatoa wito kwa wagombea wenye umri wa miaka 21 au zaidi wanaotaka kugombea nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji ,Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji wanahimizwa kuchukua fomu za kugombea katika Ofisi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Siha Christopher Timbuka amewataka Viongozi hao wa Dini kwenda kutoa Elimu kwa waumini hao katika nyumba za Ibada ili waweze  kujitokeza kujiandikisha kwenye daftrari la Mkazi pamoja na kuhakiki majina yao na ifikapo November 27 waweze kwenda kupiga kura na kuwachachua viongozi watakao watumikia kwa kipindi cha miaka 5.

Sanjari na hayo Mkurugenzi Mnasi amesema kwa Mujibu wa Kanuni ya 27,Namba 571 Kampeni za Uchaguzi zitaanza Tarehe 20 hadi Tarehe 26 November 2024 na kampeni hizo zitafanyika kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 Kamili jioni.


Related Posts