WANAHARAKATI huru nchini Tanzania wameamua kuvunja ukimya na kuwakemea na kuwaonya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wamekuwa wakianzisha chokochoko na kuhamasisha maandamano yasiyo na tija kwa Watanzania.
Pia wanaharakati hao wamekitaka Chama hicho pamoja na viongozi wao kuhakikisha R4 za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wanazitumia vizuri badala ya kuzitumia 4R kuleta vurugu wakati nchi imetulia na Serikali imeendelea kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi ya maendeleo.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wanaharakati hao wamesema chini ya Rais Dk.Samia nchi imeendelea kupiga hatua kimaendeleo na kubwa zaidi amani na utulivu upo wa kutosha lakini wanasikitishwa na viongozi wa CHADEMA ambao wamekuwa na kauli za kutaka kuvuruga utulivu kwa kuhamasisha maandamano.
“Hawa viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe wamekuwa watu wa kuhamasisha vurugu kupitia matendo na matamko yao. Hata hivyo tunawapongeza wananchi kwa kumheshimu Rais Samia kwani hawakuingia barabarani kuandamana,Mbowe akajikuta yuko yeye na mtoto wake.,”amesema Ahmed Kombo wakati wa kikao chao na Waandishi wa habari.
Kombo amesema kwamba Rais Dk.Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi inakuwa salama na yenye utulivu na wananchi wameungana na Rais kwa vitendo kwa kuyapuuza maandamano ya CHADEMA yaliyotarajiwa kufanyika Septemba 23 mwaka huu.
Amewataka viongozi wa na Chama hicho kuheshimu utawala wa Sheria na wa ache kutunisha misuli bila ya kuwa na sababu za msingi.
Kombo ametumia nafasi hiyo kumpongeza na kumtia Moyo Rais Dk.Samia kwa Kazi kubwa na nzuri anayoifanya pamoja na uwepo wa kelele za kına Mbowe na kuongeza Rais ameendelea kuhubiri amani na mshikamano.
“Tunakupongeza Rais Samia endelea kuchapa kazi,Watanzania tunaimani kubwa na wewe na tunakuunga mkono.Tunajua kazi nzuri ya Rais Samia katika kuhamasisha Utalii kupitia filamu ya Royal Tour, kupitia Rais Samia watalii wameongeza, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha nchi inakuwa na amani ili Watalii waendelee kuja na nchi iingize fedha.”
Kwa upande wake Yona Joseph Yona… amesema amekuwa ndani ya CHADEMA kwa muda mrefu na anajua mambo yao mengi sambamba na kueleza jinsi alivyopitia mateso baada ya kutekwa na hata sasa alivyomua kueleza ukweli kuna baadhi ya wanaCHADEMA wanamtafuta lakini hawezi kuogopa na ataendelea kusema ukweli.
Akizungumza kuhusu 4R za Rais Samia Yona amesema Rais ni muungwana na anaamini katika maridhiano lakini CHADEMA wanatumia fursa hiyo kufanya vurugu za kutengeneza taharuki kwa wananchi.
Amefafanua CHADEMA wanategemea misaada na msaada mkubwa wanapata kutoka nje ya Tanzania ambako kuna nchi wamekuwa wakikisaidia Chama hicho na fujo wanazofanya wanajenga uhalali wa kupata fedha hizo.
“İli wao ate fedha wanatakiwa kufanya fujo na chokochoko, pamoja na yote CHADEMA kupitia maridhiano wamejengewa ofisi na wamepewa fedha za ruzuku lakıni cha kusikitisha wakebadilika na wanachokifanya ni kuhamasisha fujo.
Amesisitiza kwa kuwa wakifanya fujo wanalipwa ndio maana hata baadhi ya viongozi wao wameacha familia nje ya nchi na huko wanalipwa, hivyo kufanya fujo kwao kunawafanya walipwe fedha.
“4R za mama zimekuja kwa nia njema lakini wameamua kutumia vibaya Uhuru waliopewa na mheshimiwa Rais .Sasa sisi kama wanaharakati huru hatuwezi kukubali na tunamwambia Rais Samia hawa watu atuachie tushughulike nao.”