Wateja wa Airtel Money kunufaika na Kampeni ya Jiboost, kujipatia sh. 20,000

 Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba akizungumza wakati wa uzinduzi  wa kampeni ya JiBoost na Airtel Money  ambayo inaleta thamani kwa wateja wao. Kampeni hiyo imezinduliwa leo Septemba 26, 2024 jijini Dar Es Salaam.

akizungumza wakati wa uzinduzi  wa kampeni ya JiBoost na Airtel Money  ambayo inaleta thamani kwa wateja wao. Kampeni hiyo imezinduliwa leo Septemba 26, 2024 jijini Dar Es Salaam.

KATIKA jitihada endelevu za kuboresha huduma za mawasiliano kwa wateja wetu nchini, Airtel Tanzania leo Septemba 26, 2024 imezindua promosheni mpya ya ‘JiBoost na Airtel Money’ ambayo inawapa nafasi watumiaji wa Airtel Money kujipatia shilingi 20,000 taslim ya supa bonasi kupitia miamala ya kila siku watakayofanya. Mpango huu ni sehemu ya maono ya kampuni ya Airtel kupanua huduma ya Airtel Money na kujenga huduma za kifedha jumuishi na wezeshi kwa wateja wake.

Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba akizungumza wakati wa uzinduzi,  wa Kampeni hiyo amesema kuwa kampeni ya JiBoost na Airtel Money ni kuleta thamani kwa wateja wao.

“Promosheni hii imetengenezwa kuwazawadia wateja wetu kila wanapotumia huduma za Airtel Money katika Maisha yao ya kila siku kama manunuzi ya vifurushi vya muda wa maongezi, intaneti, au malipo ya serikali kama vile LUKU. Wateja wetu watakuwa wakinufaika zaidi na kila muamala watakaofanya. Tunajivunia kuwa vinara wa kutoa huduma suluhishi kupitia Airtel Money kwa wateja wetu.”

Ameeleza kuwa Airtel Money siku zote imekuwa ikirahisisha maisha. Jiboost inakupa wepesi wa kufanya miamala pamoja na kurejeshewa fedha kwenye akaunti yako. Hii ni fursa ya watu wote ya kutunza na kupata fedha wakati wakiendelea kufanya matumizi.

Kwa upande wake, Balozi wa Airtel, Lucas Mhavile Maarufu kama Joti ambae alivaa uhusika wa Mr Money, amesema “Kama Mr. Money, naweza kukuambia kuwa kampeni hii ni mahususi kwa ajili ya kurudisha pesa kwenye mfuko wako. Kila utakapofanya malipo ya TV, umeme na kununua muda wa maongezi, unakuwa unajipa nafasi kubwa zaidi ya kupata bonasi. JiBoost ipo hapa kwa ajili ya kufanya miamala yako ya kila siku iwe ya furaha na yenye zawadi.”

Kampeni ya JiBoost ya Airtel Money inamruhusu Mteja kuweza kupata supa bonasi ya shilingi 20,000 kupitia muamala unaotumwa Kwenda kwa mtu mwingine, kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi, malipo ya LUKU, malipo ya serikali na kununua vifurushi vya king’amuzi. Wateja pia wanaweza kupata bonasi hiyo kwa kufungua App ya Airtel Money.

Kila mteja atakapokamilisha muamala unaostahili, atapokea ujumbe wa maandishi ukithibitisha kuwa amepata bonasi. Kila mteja atakapokuwa akifanya malipo atakuwa anapata gawio la bonasi hadi itakapofikia thamani ya shilingi 20,000. Kila bonasi atakayopata mteja itaonekana kwenye akaunti yake ya Airtel Money ikiambatana na ujumbe wa SMS utakaoonyesha mwenendo wa bonasi hizo.

Ili kuweza kunufaika na ofa hii, wateja wa Airtel wanaweza kupiga *150*60# au kutumia App ya MyAirtel kukamilisha miamala na kuanza kujizolea bonasi kupitia kampeni ya JiBoost na Airtel Money.

Related Posts