MAONYESHO YA KUKU KUFANYIKA OKTOBA.

           

Katibu wa Chama za wadau wa uzalishaji wa vifaranga Tanzania (TCPA), Alpha Ibrahimu akielezea namna  maonyesho hayo yatakavyotoa  fursa kwa wafugaji wote Tanzania akiwa na  Sufia Zuberi Katibu wa TAFM pamoja na Grace Urassa, Mkurugenzi aa Audken Farm.

 ….Na mwandishi wetu…………..

Wadau wa Tansia  ya ndege wafugwao waliopo chinu ya Taasisi ya Poultry Associatio  of Tanzania (PAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Nyama Tanzania  (TBM) wameandaa  maonyesho  ya kimataifa ya Ndegu wafugwao yatakayofanyika  oktoba 18 na 19 mlimani city jijini Dar es salaam.

Aidha Sambamba na Maonesho hayo  kutakuwepo na semina za mada mbalilmali zinazohusiana na Tasnia ya Ndege wafugwao

Akizungumza na waandishi wa Wahabari, Sufia Zuberi Kutoka Jumuiya  ya wazilishaji wa  vyakula vya mifupo Tanzani(TAFMA) amesema maonyesho hayo  ni ya nane  kufanyika yanatakuwa yakimatai kwa maana yatakutanisha nchi mbalimbali.

“Tunategemea kupata wadau mbalimbali kutoka nchi tofauti duniani ikiwemo Ubeligiji, ufaransa, Marekani, Uhalanzi, China , India pamoja na Kenya na uzuru ni kwamba makampuni ya ndani yatashiriki kuweza kujifunza vitu mbali mbali kuhusu ufugaji” amesema Zuberi

Ameongeza kuwa Walengwa wa Maonesho hayo ni watakuwa wadau wanaoshiriki katika mnyororo wa thamani wa ndege wafugwao ambao ni  watotoleshaji wa  vifaranga, Wafugaji wa kuku w Nyama, Wafugaji wa kuku wa mayai,  Watengenezaji wa vyakula vya mifugo hususani vyakula vya kuku,Wachakataji wa mazao yatokanayo na ndege wafugwao

Zuberi amesema katika maonyesho haya hakutakuwa na kiingilio na yatambana na Utoaji wa Elimu kupitia semia zitakazo fanyika kwa siku hizo mbili.

Kwa upande wake Katibu wa Chama za wadau wa uzalishaji wa vifaranga Tanzania (TCPA), Alpha Ibrahimu amesema maonyesho hayo yatatoa fursa kwa wafugaji wote Tanzania kuja kupata taarifa sahii elimu na kujifunza maendeleo ya teknolojia yalikuwa kwenye sekta ya ufugaji

“Hii fursa ambayo inakuja kwa mfugaji moja kwa moja ya kuweza kukutana na watu ambao watawapatia mahitaji yao katika ufungaji ikiwemo mayai,vifaranga na vifaa vinavyotumika katika ufugaji wakutane nao ili kama wanamaswali ya kuliza wanaweza kupata msaada kwenye maonyesho hayo” amesema ibrahim.

Ameongeza kuwa kwa Nchi ya Tanzania matumizi  na unalaji wa kuku na mayai  haupo kwa wingi sana hivyo maonyesha haya yatasaidia kuelemisha wananchi kuhusiana na ulaji wa kuku wa kisasa na Mayai na kuwa hayana madhara yotote.

Nae Grace Urassa,  Mkurugenzi  wa Audken Farm wazalishaji wa mayai Amesema wao watakuwepo kwajili ya kulitangaza yai ambalo linasadia sana kuongeza wingi wa protini katika mwili na pia kuwaeleza watanzania kuwa bidhaa tunazozalisha watanzania ni salama kwa mlaji na hazina madhara yoyote yale.

“Tunashirikiana na watu ambao tunafanya nao kazi na hivyo virutubisho tunavichukua kwao ni vitu ambavyo vinatusadia kuongeza virutubisho ambavyo vinachukuliwa vitu kama mchicha na nafaka zingine zinatengeza kwa pamoja na kupata unga ambao ndio wanaopewa wale kuku wanaokaa ndani kufugwa kama virutubisho ukiachana na yule ambao virutubisho hivyo anajitafutia mwenyewe” amesema Urassa

Kwa Upande wake Lucy Masanga, Mtaalam wa Mifugo kutoka kampuni ya Thrischool Exim Limited amesema anawakaribisha wadau wote wa mifugo kushiriki katika maonyesho hayo kwani watajifunza na kupata Elinu namna bora ya kufanya ufugaji wa kuku wa mayai na nyama.                                                                                              

Maonesho ya Ndege wafugwao yalianza mwaka 2015 jijini Dar es Salaam na mwka huu 2024 yatakuwa Maonesho ya nane kufanyika.

Related Posts