Miaka 60 ya maadhimisho ya hifadhi za Ruaha,mambo mazuri yanakuja

Katika muelekeo wa kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha Mkuu wa Uhifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki imewahamasisha Wananchi nchini kujenga utaratibu wa kutembelea hifadhi hiyo kwani ina vivutio vingi ikiwemo uwepo wa idadi kubwa ya tembo

 

Hamasa hiyo imetolewa leo katika mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Utalii zilizopo katika Manispaa ya Iringa huku akisema kuwa hifadhi hiyo imeendelea kulindwa kwa taratibu na kanuni za uhifadhi ambapo mpaka sasa imekuwa na hadhi ya juu.

Ole Meing’ataki amefafanua kuwa maadhimisho ya miaka 60 ya hifadhi hiyo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba Mosi mpaka Oktoba 07, 2024 ikihusisha matukio mbalimbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, Balozi Dkt. Pindi Chana.

 

Kwa mujibu wa Ole Meing’ataki, Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ilianza kupokea Watalii kidogo kidogo ambao walikuwa wanatembelea katika eneo la kambi la uwindaji lakini baadaye ilipoanzishwa hifadhi ya Ruaha ndipo Wageni wakaanza kutembelea eneo la Hifadhi

Hatahivyo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Imesema Dhana ya Ushirikishaji wa Jamii Katika Masuala ya Uhifadhi Imekuwa na Matokeo Chanya na Hasa Kupunguza Matukio ya Ujangili Hali Iliyosaidia Ongezeko la Wanyama Waliokuwa Hatarini Kutoweka.

 

Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Yanajumuisha Shughuli Mbalimbali Ikiwamo Makundi Tofauti Kutembelea Vivutio vya Utalii, Kongamano la Kujadili Kuhusu Historia, Mafanikio na Mwelekeo wa Hifadhi.

Shughuli Nyingine ni Kuzindua Zao Jipya la Utalii Ndani ya Hifadhi Hiyo Ambalo ni Utalii wa Puto (Balloon Safaris).

Related Posts