Polisi waeleza madhara ya dawa za kulevya katika mbio za Mwenge

Polisi Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera umetoa elimu na maelezo ya madhara ya dawa za kulevya kwa vijana wilayani humo katika viwanja vya vya Posta ambapo Mwenge wa Uhuru umepita huku wakitoa taarifa kwa Mkimbiza mwenge kitaifa namna ambavyo wamekuwa wakiendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kukabiliana na changamoto hiyo.

Akitoa maelezo mbele ya kiongozi wa Mbio za mwenge wa huru kitaifa Bwana Godfrey Mnzava ambaye aliwasii Jeshi hilo kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi Juu ya madhara ya dawa hizo.

Mkaguzi wa Msaidizi wa Polisi A/INSP Olipa Chitongo ambaye alisoma taarifa iliyoeleza namna ya mapambano dhidi ya dawa hizo Wilayani humo ameeleza kuwa kupitia mihadhara mbalimbali wamekuwa wakitoa elimu ya madhara ya dawa hizo huku wakiendelea kuwakamata wale wote wanaendelea kutumia na kuuza dawa hizo za kulevya.

Ameongeza kuwa kwa kutambua changamoto zinazowakabili vijana na makundi mengine katika jamii juu ya madhara ya dawa hizo wamkuwa wakiungana na taasisi na vyombo vya habari katika kutoa elimu kwa vijana wanaojihusisha na dawa hizo ili kuacha na kufanya shughuli halali zitakazowaiingizia kipato na kuongeza uzalishaji wilayani humo.

Related Posts