Risasi, Kahama Sixers kukiwasha fainali

LIGI ya Kikapu Mkoa wa Shinyanga imefikia patamu wakati Risasi na Kahama Sixers zikitarajiwa kuchuana katika fainali ya ligi hiyo itakayopigwa Oktoba 6, mwaka huu.

Risasi na Kahama Sixers zilitinga hatua hiyo baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Veta na B4 Mwadui mtawalia.

Katika mchezo wa kwanza, Risasi iliifunga Veta kwa pointi 92-80 na mchezo wa pili ikashinda 68-59, huku  Kahama Sixers iliishinda B4 Mwadui kwa pointi 80-75 na mchezo wa pili ikashinda 68-59.

Akiongea na Mwanaspoti kwa simu kutoka Shinyanga,  kamishina wa ufundi na mashindano wa ligi ya kikapu mkoa huo, George Simba alisema mfumo utakaotumika katika fainali hiyo ni wa timu kucheza mara tatu ‘best of three pray off’.

“Timu itakayoshinda mara mbili mfululizo itatawaza  kuwa bingwa mwaka huu  kwa ushindi wa  michezo 2-0,” alisema Simba.

Nyota wa Risasi Yohana Wiliamu, alisema timu yake imejipanga vizuri kutetea kombe lake.

“Sisi tunawajua vizuri Kahama Sixter na mkakati tuliouweka ni kuhakikisha tunashinda katika michezo yote miwili,” alisema Simba.

Related Posts