TANGA KUZINGATIA 4R ZA RAIS SAMIA KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024


 

Na Oscar Assenga,Tanga.

MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mhandisi Juma Hamsini amesema kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu utazingatia 4R za Rais Dkt Samia Suluhu.

Mhandisi Hamsini aliyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari ofisini kwake kuelekea kwenye uchaguzi huo ambapo alisema kwa Jiji la Tanga kuna mitaa 181 na kata 27 huku akiwataka wananchi kujitokeza kwenye uchaguzi hizo.

Alisema kwamba katika uchaguzi ni lazima uangalia tathimini za chaguzi zilizopita lakini wa mwaka huu utakuwa huru ,Haki na Amani .

“Lakini niwaambie kwamba Rais Dkt Samia Suluhu amehakikisha bajeti yetu tulioomba tumepatiwa kama ilivyokusudiwa hii inaonyesha uchaguzi huo ni huru na haki “Alisema

Aidha alisema kwa sababu mpaka leo hakuna mdau yoyote wa uchaguzi aliyesema anajitoa kwenye uchaguzi tofauti na ilivyokuwa mwaka 2019 kwenye uchaguzi kama huo.

“Lakini niseme kwamba kuelekea kwenye uchaguzi huo kutakuwa na vikao vya nje vya hamasa kuwahamisha wananchi kujitoeza kwenye uchaguzi pamoja ana viongozi wa Serikali na wanasiasa kuwahamisha wananchi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali,kujitokea kupiga kura”Alisema Mkurugenzi huyo

Alisema ili uchaguzi uweze kuwa mzuri lazima kuwe na uwiano sawa kwa wadau wote wanaoshiriki uchaguzi kupitia vyama vyote kuanzia kwenye ngazi ya Mtaa,Kata mpaka Halmashauri washirikishwe kikamilifu nao wanafanya hivyo.

Hata hivyo aliwaeleza wananchi kwamba uchaguzi huo unasimamiwa na Tamisemi hivyo ni muhimu kila mkazi ajiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura huku akieleza kila mgombea kwenye mtaa lazima kuwepo na nafasi za wajumbe ili mwenyekiti awe kamilifu lazima awe na wajumbe wake na Katibu wake ni Mtendaji wa Mtaa.

Related Posts