TANROADS yaeleza mafanikio makubwa iliyopata katika kipindi cha miaka 3 ya utawala wa Serikali ya Awamu ya 6

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), imesema inafanya usanifu wa kina na usimamizi wa Ujenzi wa Viwanja vya ndege, Madaraja na Barabara kulingana viwango vinavyohitajika .

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombin Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Ephatar Mlavi wakati akizungumza na waandishi wa Habari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari hii leo Septemba 26,2024 amesema juhudi za TANROAD hivi sasa ni kuhakikisha inaimarisha miundombinu yote ya barabara.

“Tunatambua umuhimu wa kuwa na vifaa vya kisasa ili kuhakikisha miradi yetu inakwenda kwa kasi na kwa ubora wa hali ya juu kufanikisha malengo ya kuimarisha miundombinu ya usafirishaji nchini”

Sambamba na hilo Mhandisi Mlavi ametoa wito kwa wananchi nchini kulinda na kuhifadhi miundombinu ya barabara na kuwataka viongozi katika maeneo yao kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kujihusisha na uharibifu wa miundombinu ya barabara.

“Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imefanya kazi kubwa katika kurejesha hali ya miundombinu baada ya kukumbwa na adha ya mvua za El-nino na kimbunga Hidaya, pia katika ilani ya ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) daraja la Jangwani limesanifiwa na mkataba wake wa ujenzi utasainiwa hivi karibu kabla ya mwezi Agosti 2024 kuisha” -Mhandisi Mlavi

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika kipindi hicho, TANROADS imefanikiwa kukamilisha miradi 38, ikijumuisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 1,198.5, madaraja makubwa tisa, na viwanja vya ndege saba katika mikoa 17.

“Kilomita 15,343.88 za barabara ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji, ambapo kilomita 1,198.50 zimekamilika kwa kiwango cha lami, na kilomita 2,031.11 ziko kwenye hatua za ujenzi. Aidha, upembuzi yakinifu wa kilomita 2,052.94 za barabara na madaraja mawili umekamilika kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami,” alisema Mlavi.

Mikoa iliyofaidika na miradi hiyo ni pamoja na Simiyu, Arusha, Dar es Salaam, Geita, Pwani, Tabora, Songwe, Ruvuma, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Iringa, Katavi, Kigoma, Mara na Mbeya.

Upande wa Wakandarasi wa ndani, amesema TANROAS inajikita katika kujenga Uwezo wa Makandarasi Wazawa, kutenga asilimia kumi (10) ya bajeti ya kila mwaka ya maendeleo kwa ajili ya Miradi ya mafunzo kwa vitendo, kutenga angalau asilimia thelathini (30) ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya upendeleo kwa wazawa.

Kuhusu makundi maalum, amesema, halikadhalika, TANROADS inajikita katika kutenga angalau asilimia tano (5) ya bajeti ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya makundi maalum bila kuacha ushiriki wa wanafunzi na wahitimu katika miradi, na kazi za matengenezo ya barabara na madaraja zitekelezwe na Makandarasi Wazawa na kusimamiwa na Washauri Elekezi Wazawa tu.

Related Posts