Watu 12 wafariki dunia na wengine 23 wakijeruhiwa ajali ya Fuso

Mbeya. Watu 12 wamefariki dunia na wengine 23 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo Septemba 27 wilayani Mbeya mkoani hapa.

Ajali hiyo imetokea eneo la Jojo Kata ya Ilembo wilayani humo,  ikihusisha gari aina ya Fuso ambayo ilikuwa ikielekea kwenye soko kwa ajili ya mnada.
Mmoja wa mashuhuda katika eneo hilo, Elias Shiwiwi amesema gari hilo  la Kampuni ya Chakazi likiwa limebeba wafanyabiashara kwa ajili ya mnada wa leo, lilikatika propela na kusababisha vifo kadhaa.

“Palepale wamefariki watano, baadaye wengine watano wakafia njiani wakielekea kituo cha afya Ilembo nikiwa nawaona hadi kufika kituoni hapo” amesema Shiwiwi.

Mganga mkuu wa kituo cha Afya Ilembo, Dk Philimon Irungi amethibitisha kupokea miili ya watu 11 ambapo mwingine mmoja alifariki baada ya kufika kituoni hapo.

“Eneo la tukio walifariki 11, ikatangulia miili sita kisha ikaja mitano na mmoja akafariki wakati akipatiwa matibabu, majeruhi ni 23” amesema Dk Urungi. 

Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii

Related Posts