Askofu Shoo: Kanisa litaendelea kupiga vita haki za watu zinapokanyagwa

Arusha. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Fredrick Shoo amesema kanisa litaendelea kushirikiana na Serikali na kupiga vita pale wanapoona haki za watu zinakanyagwa.

Aidha amesema ili mikoa nchini iendelee kukua ni wajibu wa Serikali kuweka miundombinu na kuwaachia sekta binafsi kufanya biashara bila kuwaingilia au kuwabughudhi kwa namna yoyote ile.

Askofu Shoo ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 29, 2024 alipokuwa akizungumza katika ibada ya kumstaafisha Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dk Solomon Massangwa (ambaye ametumikia kanisa kwa miaka 42), ibada iliyofanyika Usharika wa Kimandolu.

Katika ibada hiyo imehudhuriwa na maaskofu mbalimbali na viongozi wa mkoa wa Arusha akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda na Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo.

Askofu Shoo amesema wataendelea kushirikiana na Serikali na kupiga vita pale wanapoona haki za watu zinakanyagwa, kuelimisha watu kupiga vita ushirikina wa namna yoyote na kuwa hilo jukumu la watu wote kushirikiana kukemea masuala hayo.

“Sisi tutaendelea kushirikiana na Serikali, tutaendelea kupiga vita pale pote ambapo tunaona haki ya watu inakanyagwa, tutaendelea kuelimisha watu na kupiga vita ushirikina wa namna yoyote ile na tunaona mambo mengi na balaa nyingi zimekuja katika nchi hii kwa sababu, ushirikina huu,” amesema Askofu Shoo.

“Kwa bahati mbaya sana wako hata viongozi wa ngazi za juu sana ambao wanashiriki katika matendo kama hayo kwa sababu imani zao za kishirikina zimewaongoza kwamba eti ili cheo kipande au upate nafasi fulani lazima uingie kwenye matendo ya namna hiyo,” amesema.

“Ni wajibu wetu viongozi wa dini tushirikiane na viongozi kama ninyi wa Serikali kukemea mambo haya, amesisitiza Dk Shoo

Shoo ambaye pia ni Mkuu mstaafu wa KKKT, amesema wanaona mkoa wa Arusha unavyofufuka na kupiga hatua kubwa kiuchumi na kuwa ni muhimu sana ili mikoa na mingine nchini ipige hatua ni wajibu wa Serikali kuweka miundombinu, iwaachie sekta binafsi kufanya biashara na wasingiliwe  au kubughudhiwa kwa namna yoyote ile.

“Arusha imekuwa hivi kwa sababu ina watu wabunifu na wachapakazi na hawa watu wanaleta uchumi sasa Serikali iwatie moyo kuwaachia wafanye baishara zao bila kubughudhiwa au kunyanyaswa kwa namna moja au nyingine,” amesema

Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, Askofu Shoo amesema wao kama viongozi wa dini katika umoja wao wamekuwa waaminifu wakiwakumbusha waumini juu ya kujiandikisha na kushiriki kwenye mchakato huo muhimu.

Naye Askofu Dk Godson Mollel wa Dayosisi ya Kaskazini Kati aliyechukua nafasi ya Dk Massangwa amesema suala la Hospitali ya Selian linaendelea kushughulikiwa kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya.

“Niliambie kusanyiko hili hatua zimeendelea na sasa liko Wizara ya Afya, kwa amelekezo tunalifuatilia hatulali, nishukuru uongozi wa nchi kuanzia ngazi za juu kwa kulisukuma suala hili,”

“Tunashukuru watumishi wa hospitali kwa uvumilivu uliopitiliza, baada ya kumaliza jambo hili tunaanza juhudi katika suala hilo la hospitali na kwa kuwa tunaenda pamoja na Serikali, tunaamini Mungu atatufikisha najua tutatoboa,” amesema Dk Mollel.

Akitoa salamu zake kanisani hapo, Gambo amesema wakati anasimikiwa Dk Godson Mollel, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aliahidi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kuweka lami kutoka barabarani hadi kanisani hapo.

“Nimekwambia wewe pia kwa sababu masuala ya barabara yako chini yako, tusaidie chini ya Tarura kabla ya uchaguzi tuwe tumepata barabara,” amesema.

“Ombi langu la pili, wakati tunamzungumzia Dk Masangwa, tunamzungumzia alama aliyoacha katika hoteli ya Corridor Spring ambayo ilipata misukosuko, naiona changamoto hiyo kupitia Hospitali yetu ya Seliani,” amesema, akikazia alichokisema Askofu Mollel.

“Ni hospitali ambayo imepata changamoto kubwa na lazima Serikali tuondoe dhana ya kushidnana na hospitali binafsi kwa sababu wote wanahudumia Watanzania. Ni  imani yangu kupitia ofisi yako (RC) nafahamu umahiri wako, hili litaisha,” ameongeza.

Akijibu hoja hizo, Makonda amesema atawasilisha ngazi za kitaifa juu ya ubovu wa barabara na wiki ijayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa atakuwa ziarani mkoani humo na moja ya barabara zitakazojengwa ni hiyo ya kuelekea kanisani.

“Barabara nyingi za Arusha ni mbovu sana na shida yetu kubwa ni uongozi mkoani na wilayani vita zao za kisiasa, majungu waganga wa kienyeji hawapigi hatua,”amesema Makonda

Katika maelezo yake kanisani hapo, Makonda amesema viongozi wa dini ni msingi mkubwa wa amani na utulivu katika taifa lolote linaloamini katika Mungu.

“Pamoja na Serikali inasema haina dini, lakini madam viongozi wake wana imani, basi imani hizo huhuisha upendo, umoja na hatimaye kufanya kazi pamoja bila kujali kabila,udini na kuwahudumia wananchi bila kubagua walipotoka,” amesema.

“Nimepata faraja kumuona Dk Shoo, nampongeza kwa kazi kubwa aliyofanya kwanza akiwa Askofu Mkuu wa KKKT. Nimuombe busara zako ziendelee kwa kuwa Mungu alikupa kibali cha kitaifa na mataifa basi popote unapoona jambo usisite kutupa hekima zako ili tuendelee kusonga mbele,” amesema

Makonda alimpongeza Dk Massangwa kwa kuwa miongoni mwa waliochangia kujenga amani, umoja na mshikamano katika mkoa wa Arusha

Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakidhulumiwa na miongoni mwa wanaofanya hivyo ni baadhi ya viongozi na kuomba kanisa kusimama katika nafasi yao.

Kuhusu mgogoro wa wafanyakazi wa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center (ALMC), maarufu kama Selian inayomilikiwa na kanisa hilo, Makonda amesema wakati wa kliniki walipata mgomo wa madaktari uliokuwa unaendelea na kuwa walishawasiliana na Mkuu wa Kanisa hilo, Dk Alex Malasusa na kulishughulikia.

“Tunashukuru watumishi wa hospitali kwa uvumilivu uliopitiliza, baada ya kumaliza jambo hili tunaanza juhudi katika suala hilo la hospitali na kwa kuwa tunaenda pamoja na serikali, tunaamini Mungu atatufikisha najua tutatoboa,” amesema Dk Mollel.

Akitoa salamu zake kanisani hapo, Gambo amesema wakati anasimikiwa Dk Godson Mollel, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aliahidi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kuweka lami kutoka barabarani hadi kanisani hapo.

“Nimekwambia wewe pia kwa sababu masuala ya barabara yako chini yako, tusaidie chini ya Tarura kabla ya uchaguzi tuwe tumepata barabara,” amesema.

“Ombi langu la pili, wakati tunamzungumzia Dk Masangwa, tunamzungumzia alama aliyoacha katika hoteli ya Corridor Spring ambayo ilipata misukosuko, naiona changamoto hiyo kupitia Hospitali yetu ya Seliani,” amesema, akikazia alichokisema Askofu Mollel.

“Ni hospitali ambayo imepata changamoto kubwa na lazima serikali tuondo dhana ya kushidnana na hospitali binafsi kwa sababu wote wanahudumia watanzania,ni imani yangu kupitia ofisi yako (RC) nafahamu umahiri wako, hili litaisha,” ameongeza.

Akijibu hoja hizo, Makonda amesema aliwahawasilisha ngazi za kitaifa juu ya ubovu wa barabara na wiki ijayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa atakuwa ziarani mkoani humo na moja ya barabara zitakazojengwa ni hiyo ya kuelekea kanisani.

“Barabara nyingi za Arusha ni mbovu sana na shida yetu kubwa ni uongozi mkoani na wilayani vita zao za kisiasa, majungu waganga wa kienyeji hawapigi hatua,”amesema Makonda

Katika maelezo yake kanisani hapo, Makonda amesema viongozi wa dini ni msingi mkubwa wa amani na utulivu katika taifa lolote linaloamini katika Mungu.

“Pamoja na Serikali inasema haina dini, lakini madam viongozi wake wana imani, basi imani hizo huhuisha upendo, umoja na hatimaye kufanya kazi pamoja bila kujali kabila,udini na kuwahudumia wananchi bila kubagua walipotoka,” amesema.

“Nimepata faraja kumuona Dk Shoo, nampongeza kwa kazi kubwa aliyofanya kwanza akiwa Akosfu Mkuu wa KKKT. Nimuombe busara zako ziendelee kwa kuwa Mungu alikupa kibali cha kitaifa na mataifa basi popote unapoona jambo usisite kutupa hekima zako ili tuendelee kusonga mbele,” amesema

Makonda alimpongeza Dk Massangwa kwa kuwa miongoni mwa waliochangia kujenga amani, umoja na mshikamano katika mkoa wa Arusha

Makodna amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakidhulumiwa na miongoni mwa wanaofanya hivyo ni baadhi ya viongozi na kuomba kanisa kusimama katika nafasi yao.

Related Posts