Humoud apewa miwili Zambia | Mwanaspoti

Mtanzania Abdulrahim Humoud amesema ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia Konkola Blades FC baada ya ule wa awali kutamatika msimu uliopita.

Humuod alisaini mkataba wa miezi sita ambao ulitamatika msimu uliopita akitokea Namungo ya nchini Tanzania.

Akizungumza na Nje ya Bongo, Humuod alisema alipewa mkataba mfupi kwa lengo la kumuangalia lakini baada ya kuonyesha kiwango bora wakampatia mkataba wa miaka miwili.

“Nikweli nilikuja hapa nikapewa mkataba wa miezi sita kitu kizuri nilitumia vizuri muda niliopewa, kila nikipata nafasi ya kucheza nilionyesha kiwango bora, hapo ndio waliamua kunipa mkataba mpya na kufanya kila kitu ambacho nilihitaji ili nibakie kwenye timu kwasababu kuna ofa nyingine tayari zilishajitokeza,” alisema Humuod na kuongeza

Kuhusu ugumu wa nafasi ya kucheza hasa kwenye eneo la ulinzi ambalo anacheza alisema sio rahisi kutokana na ushindani wa mabeki ambao wapo takribani saba na wote wazuri.

“Ugumu upo kwa sababu  ni mgeni na wazawa waliopo kwenye nafasi yangu wote ni wachezaji wazuri tupo saba katika eneo hilo, lakini kwa sababu nimemua kufanya kazi nakufata maelekezo ya Kocha basi napata nafasi ya kucheza kila mechi.”

Baadhi ya timu alizozichezea beki huyo ni Ashanti United (2007/08), Mtibwa Sugar (2008–2010), Simba (2010/2011), Azam FC (2011–2013),    Simba(2013/2014), Sofapaka (2014), Coastal Union (2014–2016), Real Kings (2016/2017), Malindi (2017), KMC FC (2018), Arusha United (2018–2019), Mtibwa Sugar (2019).

Related Posts