KOCHA aliyewahi kuifundisha Yanga msimu 2020, Luc Eymael ametambulishwa kwenye kikosi cha FC Lupopo ya DRC Congo anakochezea mtanzania, Abdallah Shaibu ‘Ninja’.
Lupopo hivi karibuni waliondolewa katika raundi ya pili ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho CAF dhidi ya Bravos ya Angola kwa mabao 2-1 hali iliyosababisha klabu hiyo kumfuta kazi kocha Mohamed Magassouba wa Malina.
Akimuelezea kocha huyo Ninja alisema ni kweli ametambulishwa na tayari amehudhuria mazoezini siku mbili.
Ninja alisema wakati kocha huyo anajiunga na Yanga hakuwepo kikosini ingawa alifanya nao mazoezi kwa siku mbili wakati huo alikuwa Marekani.
“Nahisi hanikumbuki kwa sababu wakati yeye anakuja Yanga mimi nilikuwa natoka na ndio kipindi alichofungiwa miaka miwili sijamfahamu sana lakini kwa kuwa yupo hapa itakuwa rahisi,” alisema Ninja.
Kabla ya Lupopo alifundisha Yanga, Stade Tunisien na Al-Ettihad, Al-Misraty Club.