MBUNGE JIMBO LA SEGEREA KUWAUNGA MKONO WASICHANA WENYE TAALUMA MBALIMBALI

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Dar es Salaam Bonah Kalua ameahidi kuwaunga mkono wasichana wenye taaluma mbalimbali za masuala ya urembo na upishi katika mwanzo mpya wa kujijenga kibiashara.

Kalua ametoa ahadi hiyo kwa wahitimu wa kozi za urembo ikiwemo ususi, ushonaji, upishi wa keki na urembo wa ngozi (make-up) wa chuo cha Lisa College kwenye sherehe za mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Kinyerezi – Songas, Dar es Salaam.

“Ni muhimu sana kuwa na chuo kama hiki katika jimbo letu na hii inatoa fursa kubwa kwa vijana kupata ujuzi wa hali ya juu ambao unawapeleka moja kwa moja katika kujitegemea kibiashara hivyo kuongeza wigo wa wachangiaji ukuaji wa uchumi wa nchi sambamba na wazaslishaji wa ajira mpya na hili nitaliunga mkono kwa namna ya pekee ili wahitimu hawa na wengineo wawe chachu ya maendeleo ya taifa letu”.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho, Lisa Deus amesema “Unapokuwa na jamii ya watu wenye ujuzi wa kuweza kuanzisha biashara zao binafsi unaipunguzia serikali mzigo wa kuajiri na badala yake unatengeza ajira mpya ambazo serikali itanufaika zaidi kwa kuongeza wigo wa wajasiriamali na walipa kodi”.

Bara la Afrika limekuwa likikabiliwa na changamoto ya uchache wa ajira rasmi hususani kwenye taasisi za umma na binafsi zinazotambulika hivyo kuzilazimu serikali za nchi hizo kuhimiza wawekezaji wakiwemo wa ndani kuanzisha shughuli zinazochangia ukuaji wa ajira ikiwemo uendeshaji wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya ya ujuzi yanayosababisha wahitimu kuanzisha ajira binafsi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa chuo hicho, Lisa Deus wahitimu hao wanapewa fursa ya kuanzisha biashara chini ya usimamizi wa chuo hicho kwa kukopeshwa mitaji ya vifaa na vitendea kazi sambamba na kuunganishwa na wateja ili kukuza biashara zao.




Related Posts