MBUNGE wa Jimbo la Ukonga na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, amefanya ziara ya kutembelea soko la Chanika leo Septemba 29, 2024, ambalo lilipatwa na moto hivi karibuni.
Mhe. Silaa aliongozana na viongozi wa soko na kukagua uharibifu mkubwa uliofanyika, ambapo aliona athari za moja kwa moja kwa wafanyabiashara na jamii nzima.