Mwenge wa Uhuru wafika kwenye maradi Mkubwa wa BUWASA-Bukoba

Mwenge wa uhuru umeendelea kukimbizwa Mkoani Kagera ambapo unakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akiwa katika manispaa ya Bukoba umepitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji awamu ya pili unaotekelezwa chini ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bukoba (BUWASA) uliopo katika kata ya Buhembe ukigharimu zaidi ya bilioni 3.

Akisoma taarifa ya mradi Mhandisi Daudi Beyanga ambaye ni msimizi wa mradi huo amesema kuwa mradi ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2020 na unatarajia kukamilika Desemba mwaka huu 2024 na ukikamilika utatoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wapatao elfu kumi na nane kutoka kata tano za manispaa ya Bukoba ambazo ni Buhembe,Nyanga,Kahororo,Kashai,Nshambya na kata ya Nyakato kutoka Wilaya ya Bukoba ambao wamekuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Mzava amewapongeza BUWASA kwa hatua waliyofikia huku akiwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji na kuheshimu miundombinu inayowekwa ili mradi uweze kudumu kwa muda mrefu na kuwapunguzia wananchi changamoto ikiwa ni sambamba na kuwaelekeza BUWASA kutafuta hati ya maeneo ya mradi ili kujihakikishia usalama wa eneo hilo.

Related Posts