STRAIKA wa Henan Jianye inayoshiriki Ligi Kuu nchini China, Opah Clement amekuwa na msaada kwenye kikosi hicho eneo la ushambuliaji na kuwa tumaini kwenye kikosi hicho kilichokuwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi.
Timu ya Mtanzania huyo ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi kati ya 12 zinazocheza ligi hiyo ikikusanya pointi 19 kwenye mechi 22.
Tangu ametua kikosini hapo Agosti amecheza mechi tano akiifungia timu hiyo mabao matatu ambayo yameisaidia kuitoa mkiani na kuisogeza hadi nafasi ya 10.
Mechi yake ya kwanza baada ya kutambulishwa ilikuwa dhidi ya Yongchuan Chashan akifunga bao 1-0 lililoipa timu hiyo ushindi wa pointi tatu pekee.
Akaanza tena kwenye mechi ya pili ambayo alicheza dakika zote 90 timu yake ikiifunga Zhejiang mabao 2-1, ikapoteza Jiangsu 2-1, Shaanxi Changan 1-1, Beijing Beikong 0-0 na kupoteza dhidi ya Guangdoung 3-1.
Kabla ya kusajiliwa Opah timu hiyo ilipoteza mechi tatu na suluhu moja dhidi ya Shanghai 0-0 ikapoteza dhidi ya Shandong SL 2-1, Wuhan Jiangda 1-0, Changchun Dazhong 5-0.
Hivyo ni kama timu hiyo imepata suluhu eneo la ushambuliaji baada ya kufika kwa nahodha huyo wa timu ya taifa ‘Twiga Stars’.