Vyama vya Ushirika vyatajwa kuwa mkombozi Kwa wananchi

Vyama vya Ushirika nchini vimetajwa kuwa mkombozi katika mashirika na taasisi mbalimbali Kwa kuwaunganisha wafanyakazi na Watu wa kada zote na kuwainua kiuchumi .

Hayo yamesemwa na CPA Gabriel Msuya Kaimu Meneja Ushauri wa Coasco ambapo amesema licha ya kuwa na changamoto ndogondogo Bado ushirika umekua na mfanikio makubwa nchini.

Amesema kutokana na umuhimu huo wafanyakazi wa Vyama vya Ushirika watakiwa kufanya kazi Kwa weredi na kuzingatia maadili yanutumishi ili kuendelea kuwajengea Imani wanachama wao.

Aidha amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu ili kuendelea kupata hati safi na za kuridhisha badala ya kuzalisha migogoro ambayo imekua ikirudisha nyuma maendeleo kwenye ushirika.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu wameshukuru kwa kupata ufahamu wa matumizi mbaliy ikiwemo tecnolojia .

Wamesema watakuwa mabalozi kwa wengine ili lengo la Ushirika la kuwaunganisha na kuwainua kiuchumi wananchi linatimia.

Related Posts