WAANDISHI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZA LISHE KWA KUFUATA VYANZO SAHIHI

NA MWANDISHI WETU

WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kutafuta taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo,chombo ama taasisi husika ili kufanikisha kuandika kwa usahihi masuala yanayohusu lishe ili kufikisha ujumbe stahiki kwa wananchi pasipo kupotosha.

Ofisa Uhusiano na Mtafiti wa Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania,Hamza Mwangomela,a mebainisha hayo leo Septemba 26, 2024 jijini Dar es Salaam wakati semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika habari kwa usahihi kuhusu masuala ya lishe.

“Kuna mambo yanajitokeza hususan katika mahojiano utakuta anahojiwa mtu ambaye si sahihi na kusababisha kupotosha usahihi wa jambo husika na inapotokea hivyo tunachukua hatua za kuwaita

walihojiwa ili kufahamu wanachokijua kuhusu lishe na wengi wao tunabaini hawana elimu ya kutosha”

“Pia hatuishii hapo huwa tunawaandikia barua vyombo husika kwa hatua zaidi ili kupata maelezo ya kutosha na wale wakaidi, tunapeleka taarifa zao katika mamlaka zinazowadhibiti ikwemo, Mamlaka za Mawasiliano Tanzania (TCRA)na tunashukuru mambo yanakwenda vema,” amesema.

Mwangomela amesema jambo lingine ambalo baadhi ya waandishi na watangazaji wakosea wakati kutumia neno kirutubisho na kirutubishi litumika kwa binadamu.

Akifafanua hilo, Mwengomela amesema ” Neno kirutubisho usahihi wake ni kwamba linatumika kwenye mimea na neno Kirutubishi linatumika kwa binadamu.
Mwisho
Ofisa Uhusiano na Mtafiti wa Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Hamza Mwangomela akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha  Semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika habari kwa usahihi kuhusu masuala ya lishe jijini Dar es Salaam.

Related Posts