Walimu wa shule binafsi na za umma hakikisheni mnatoa msisitizo wa vitendo kwenye masomo ya Sayansi

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa chama CHAMA Cha mapinduzi Tanzania Bara Bw Joshua Mirumbe ametoa wito kwa walimu wa shule binafsi na za umma kuhakikisha wanatoa msisitizo ya vitendo kwenye masomo ya Sayansi kwa wanafunzi wao, ili taifa la kesho liwe na watalamu wengi wa ndani.

Naibu Katibu Mkuu wa umoja wa wazazi amesema hayo alipokuwa akikagua bunifu za wanafunzi wa shule ya sekondari ya YOHANNES katika maeneo ya umeme, maji, Sayansi na kilimo.

Pia Joshua Mirumbe amesema kuwa taifa Bado linahitaji watalamu wa ndani watakaotumika kwenye utekelezaji wa miradi ya ndani, jambo litakaloinua uchumi wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa mmiliki wa shule ya sekondari (Yohannes) Valerian Msaki amesema kuwa serikali imeendelea kuwaunga mkono kwa kuondoa Kodi ya ongezeko la thamani VAT kwenye vifaa vya kujifunzia kwa mashule binafsi na kufanya hivyo kumerahisisha hata ufundishaji kwa wanafunzi hao.

Naye mkuu wa shule hiyo Sister Wema Kabigi amesema elimu ya vitendo haitolewi kwa upande wa Sayansi pekee bali pia masomo ya sanaa na biashara.

Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu Joshua Mirumbe amewataka wazazi waendelee kuvikuza vipaji vya watoto wao baada ya kuhitimu shuleni hapo kwa manufaa yao na mafunaa ya watoto wao.

Related Posts