Waziri Silaa Awasisitiza Waumini Kujiandikisha Kupiga Kura

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Jerry Silaa amewataka viongozi wa kanisa kuwaasa waumini wao kutenga muda wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili wapate nafasi ya kushiriki kuchagua viongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Agizo hilo amelitoa leo Septemba 30,2024 katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKT Kigezi-Chanika Jijini Dar es Salaam.

Aidha amesema waumini wa kanisa wanaweza pia kuomba nafasi za uongozi,kwa lengo la kupata viongozi wenye hofu ya mungu ili kuleta maendeleo bora na ustawi wa jamii.

Pamoja na hayo amesema jukumu la uraia linajumuisha kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi kwa ajili ya wananchi wote ambapo upatikanaji wa huduma ya shule, zahanati na mengine yanahusiana na uwepo wa viongozi wanaopatikana kupitia chaguzi.



Related Posts