DC Morogoro akemea uchafu kwenye makazi na maeneo ya biashara

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Mussa Kilakala ametoa Rai kwa Wananchi na Wafanyabiashara Wilaya ya Morogoro kushiriki kwenye Utunzaji na Ulindaji wa mazingira kwenye maeneo yao ili kuufanya Mji wa Morogoro kuwa Safi na Salama dhidi ya Magonjwa ya kuambukizwa.

Ametoa Rai hiyo alivyoshiriki zoezi la Kufanya Usafi Kata ya Kihonda Maghorofani Manispaa ya Morogoro, katika zoezi hilo aliambatana na Viongozi mbalimbali wakiwemo Meya wa Manispaa ya Morogoro, Madiwani na Maafisa mbalimbali wa Serikali wilayani Morogoro.

DC Kilakala amesema usimamizi wa sheria unahitajika ili kuendeleza kuweka Mji katika Mazingira mazuri.

DC Kilakala amesema Kila mtu anawajibu wa kufanya usafi kwenye Mazingira yanayo mzunguka badala ya kusubiri Serikali ije ifanye usafi katika Maeneo yao.

Nao baadhi ya wakazi wa Morogoro wamesema Serikali inatakiwa kuwachukulia hatua za kisheria watu watakao onekana kuchufua Mazingira kwa makusudi.

Wamesema baadhi ya miji mtu akitupa Uchafu anapigwa faini ya shilingi elfu 50 lakini kwa Morogoro Bado sheria hui haisimiwi kikamilifu.

Related Posts