Kocha Mbeya Kwanza acharuka | Mwanaspoti

LICHA ya Mbeya Kwanza kupoteza michezo yote miwili mfululizo katika Ligi ya Championship, kocha mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Masawe amesema, hawakuzidiwa kwa uwezo na wapinzani wao isipokuwa wenyeji wamekuwa wakilazimisha ushindi.

Mbeya Kwanza iliyowahi kushiriki Ligi Kuu msimu wa 2021/22 kisha kushuka daraja, imeanza Ligi ya Championship kiugumu baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo, ikichapwa mabao 2-1 na Songea United kisha kupoteza bao 1-0 kwa Mbeya City.

“Waamuzi wanaamua wanavyotaka kuwabeba wenyeji, tunakubali tumepoteza mechi hizo ila sio kwa kuzidiwa, tunaenda nyumbani kuwapokea wapinzani wetu na tutashinda pia, siwezi kufanyia tathimini ya timu kwa sasa hadi tutakapofikisha michezo 10.”

Kuhusu usajili na ubora wa wachezaji, Masawe alisema anaona kikosi hicho kipo fiti kwa sababu kila mchezaji anajituma uwanjani.

“Tunarudi katika uwanja wetu wa nyumbani kujipanga upya tukiwa na malengo ya kuvuna pointi tatu, baada ya michezo minane hadi 10, ndio naweza kubaini mwelekeo wetu ila kwa sasa ni mapema kwani vijana wanaonyesha ubora wao mzuri uwanjani.”

Related Posts