Lukuvi agawagawia vijana mitungi ya gesi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu), William Lukuvi, ameendelea kuunga mkono kampeni ya kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutoa majiko ya gesi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi soka ya Kata katika jimbo la Isimani.

Ametoa majiko hayo kwa washindi wa nafasi ya kwanza, nafasi ya pili na nafasi ya tatu wakati alipotembelea Kata Mlenge mkoani Iringa Septemba 29, 2024 katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo katika vijiji vya Magombwe, Isele, Kinyika na Kisanga vilivyopo katika kata ya Mlenge.

“Majiko 1200 yanatarajiwa kutolewa kwa washindi wa mpira wa miguu kwa kata zote za jimbo la Isimani ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Mhe, Rais Dkt, Samia Suluhu Hassani katika kutumia nishati safi ya kupikia,” amesema Waziri Lukuvi.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi, ameomba wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuendelea kuunga mkono serikali utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa.

“Utakapofika muda wa uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani, naomba vijana wenye umri wa miaka 18 na kuendelea mjitokeze kujiandikisha uchaguzi wa mwakani muweze kupiga kura”,amesema.|

Related Posts