KINDA la FCA Darmstadt ya Ujerumani, Athuman Masumbuko ‘Makambo Jr ‘ amesema ameanza kuzoea Ligi na mazingira ya nchi hiyo ambayo ni maraya kwanza kwake.
Timu hiyo hadi sasa imecheza mechi tisa ikikusanya pointi 18 na nyota huyo akianza kwenye baadhi ya mechi na kufunga bao moja na assisti moja.
Makambo Jr aliliambia Mwanaspoti kuwa alipofika alipata ugumu kidogo ingawa sio sana kwa kuwa aliwahi kucheza Denmark.
Aliongeza kuwa ligi ya nchi hiyo imemfanya aanze kuwa mkomavu kwani bila ya kufanya jambo la ziada uwanjani unaweza kuambulia benchi.
“Ligi ya wenzetu haina utani yaani timu zinaingia uwanjani kushindana kweli kwahiyo kocha anahitaji wenye ukomavu ukijisahau kidogo imekula kwako tupo tunaendelea kupambana na juhudi zetu binafsi,” alisema Makambo Jr
SpVgg Neu-Isenburg 1 – 0 FCA Darmstadt
FCA Darmstadt 4 – 2 Rot-Weiss Frankfurt
Beienheim 4 – 5 FCA Darmstadt
GroB-Gerau 0 – 2 FCA Darmstadt
FCA Darmstadt 3 – 0 Kickers Offenbach II