Putin asema Urusi itatimiza malengo yote yaliyowekwa Ukraine – DW – 30.09.2024

Katika ujumbe wa maadhimisho ya miaka miwili ya kuunganishwa kwa majimbo maanne ya Ukraine kwa Urusi, rais Vladimir Putin wa Urusi ameahidi kwamba malengo yote yaliowekwa na nchi yake huko Urkaine yatafikiwa. Huku akisema ukweli uko upande wa Urusi.

“Niliamua kufanya operesheni maalum ya kijeshi. Lengo lake ni kuwalinda watu ambao wamekuwa wakiteswa na mauaji ya halaiki kutoka kwa serikali ya Kyiv kwa miaka minane.”, alisema Putin.

Kabla ya kuendelea kusema : “Kura za maoni zilifanyika katika Jamhuri za Watu wa Donetsk na Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson. Matokeo yake yanajulikana. Watu walifanya uchaguzi wao wazi. Leo tunatia saini makubaliano ya kujiunga kwa Jamhuri ya Watu wa Donetsk, Jamhuri ya Watu wa Luhansk, eneo la Zaporizhzhia na eneo la Kherson kwa Urusi.”,alisema Putin.

Katika hotuba yake, Putin aliwashutumu vikali viongozi wa nchi za Magharibi, ambao amesema wameigeuza Ukraine kuwa koloni lao na ngome yao ya kijeshi  kwa kuilenga Urusi.

Baada ya kutuma wanajeshi nchini Ukraine mnamo Februari 2022, Urusi iliteka maeneo ya Luhansk, Donetsk, Zaporizhzhia na Kherson. Lakini hata hivyo haina uthibiti kamili wa majimbo hayo.

Mshambulizi ya Droni Kyiv 

Urusi imefanya mashambulizi ya droni mapema leo katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev
Urusi imefanya mashambulizi ya droni mapema leo katika mji mkuu wa Ukraine, KievPicha: Gleb Garanich/REUTERS

Serikali ya Ukraine imeseama Urusi liushambulia mji wa Kviv kwa droni na mabomu usiku wa kuamkia Jumatatu. Jeshi la anga la Ukraine limesema lilidungua droni 73 zilizotumwa na Urusi katika kipindi cha masaa matano. Mashahidi wamesema walisikia milipuko kadhaa mjini Kyiv katika  kile kilichoonekana kama udunguaji wa droni za Urusi na mifumo ya ulinzi ya Ukraine.

Gavana wa jimbo la Kyiv Ruslan Kravchenko amesema hakukuwa na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu lakini mashambulio hayo yalisababisha moto katika wilaya tano za mkoa huo.

Wakati huohuo shirika la habari la Urusi la Interfax limesema kuwa jeshi la nchi hiyo limeuteka mji wa Nelepivka huko mashariki mwa Ukraine.

Mmarekani akiri mashtaka

Kwenye taarifa nyingine, Raia wa Marekani Stephen James Hubbard aliyekamatwa wiki iliopita nchini Urusi, amekiri mashtaka ya shughuli za mamluki katika Mahakama ya Moscow.

Shirika la habari la RIA limesema Hubbard amekiri kwamba alikuwa amepokea pesa kupigania Ukraine dhidi ya Urusi.

Ikiwa tahukumiwa Stephen Hubbard anakabiliwa na kifungo cha miaka saba hadi 15 jela.

Related Posts