Vijana tumieni mitandao ya kijamii kupongeza mazuri yaliofanywa na Serikali -MNEC ASAS

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Salim Asas amewataka vijana wote nchini kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya ya kuwaletea maendeleo wananchi ambapo amesema ni muhimu vijana kupitia mitandao ya kijamii kuwajibu wanaomchafua Rais, badala ya kutumia mitandao kujipiga picha zisizo na maana.

 

Asas amesema hayo wakati akifunga mafunzo maalum kwa vijana 370 kutoka Kata 107 mkoani Iringa yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa, na kuhitmishwa leo katika Chuo cha Ihemi.

Mafunzo hayo yaliyoanza septemba 23-yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo vijana katika kukilinda Chama na viongozi wake na yamehudhuriwa na vijana wapatao 370 kati ya 428 ya vijana wote ambao walitakiwa kushiriki, huku kila kata ikitakiwa kutoa vijana wanne ambao ni Mwenyekiti na Katibu, Katibu wa Hamasa na mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoa.

Akizungumza na vijana hao, Asas amesema wapo wanasiasa ambao wanaipotosha jamii kwa kueleza uongo juu ya utendaji kazi wa Rais Dk.Samia kwenye mitandao ya kijamii, na kuwataka vijana hao kutowafumbia macho watu wenye nia ovu na serikali wakiwemo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakisambaza maneno ya kichochezi yenye lengo la kuwachonganisha wananchi na serikali yao.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia imefanya kazi kubwa kuanzia miradi ya kimkakati na ya maendeleo kuanzia ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji kwa kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi pamoja na kutekeleza miradi mipya, hivyo ni jukumu la vijana wa UVCCM kuhakikisha wanaitumia vizuri mitandao ya kijamii kujibu upotoshaji huo kwa kusemea juu ya kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani inayofanyika.

 

 

‘’Wapinzani baada ya kuona kila wanapogusa mama kafanya, kila wanapotaka kupotosha mama katekeleza wamefilisika ajenda na hivi sasa wameamua kumchafua kiongozi wetu mkuu kwa kueneza uongo, haiwezekani tunyamaze. Na sisi tunataka asilimia 70 ya majibu ya kumtetea kiongozi wetu,hivyo vijana tunahaja ya kumsemea mama,tumieni mitandao ya kijamii kujibu upotosha unaofanywa na vyama vya upnzani’’amesisitiza Asas.

Related Posts