Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea mhandisi Chionda Kawawa amewaomba viongozi wa dini kuhamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha na kujitokeza kugombea na kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa/vijiji na vitongoji unaotakiwa kufanyika 27/11/2024.
Viongozi wa dini na Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea wapata semina ya namna gani ya kuhamasisha wananchi wajitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji

Na Fredy Mgunda, Nachingwea Lindi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea mhandisi Chionda Kawawa amewaomba viongozi wa dini kuhamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha na kujitokeza kugombea na kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa/vijiji na vitongoji unaotakiwa kufanyika 27/11/2024.
Akizungumza na viongozi hao wa dini, mhandisi Kawawa alisema kubwa viongozi wa dini wanaushawishi mkubwa kwa wananchi kuweza kujitokeza kushiriki kikamilifu katika uchanguzi wa mwaka huu.
Mhandisi Kawawa alisema kuwa serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na viongozi wa dini katika Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea hivyo zoezi hilo lipo mikononi mwao tu kwa kushirikiana na serikali.
Alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaumhimu mkubwa katika mustakabali wa maendeleo ya wananchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo hivyo ni muhimu kila mwananchi kushiriki kikamilifu uchaguzi huo.
Kwa upande wao viongozi wa dini katika Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea walisema kuwa wapo tayari kushirikiana na serikali kutoa elimu ya umuhimu wa kushiriki zoezi zima la uchaguzi kwa wananchi wote.
Walisema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kushiriki kikamilifu uchaguzi wa mwaka huu ili kuweza kuchagua viongozi wapenda maendeleo na wenye nia njema ya kuwatumikia wananchi.